Pages - Menu

Jumamosi, 24 Agosti 2013

(Photo) Leo ni kumbukumbu ya kuzaliwa FEZA KESSY












(News) The Biggest ProHabo Project 2013!



                         We Bring You Lafamilia's Chidibenz all the way from Bongo Daresalam!

                                Champagne zinaendelea..Fly Like a Jordan Air! Coming Soon
                                                           BONGE LA KIOO

(Breaking News) Hii ndio ajali iliyompata msanii huyu wa Bongo Movie jana usiku akirudi kwake


Yalikuwa ni majira ya usiku wakati Hemedy PHD anamrudisha mshkaji wake Gelly wa Rhymes home kwake Sinza ndipo mshkaji wakati anarudi kwake ndipo ikatokea hii ajali mbaya kwa kugonga kalivati lililopo pembeni ya mtaro hapa maeneo ya Kijitonyama Kisiwani. Hemedy ameumia kwenye paja na kifuani ambapo staring ilimbana, kwa sasa bado yuko hosp anaendelea na matibabu.

Jumapili, 21 Julai 2013

kutoka hospitali alipojifungua mchumba wa Mabeste


MABESTE AKIWA NA MCHUMBA WAKE LISA PAMOJA NA MTOTO WAO KENDRICK

(News) Baada ya MABESTE msanii mwingine anayetarajia kupata mtoto ni huyu....



Ni kama mwezi au miezi sasa baada ya kuuaga ukapela na kuingia kwenye maisha mapya ya ndoa, msanii anayeuwakilisha mkoa wa Mwanza anajulikana kwa jina la H-Baba nae ameongea na WAKUPENDEZAblog na kutoa habari yakuwa siku mbili hili za mbeleni ndoa yake inakaribia kujipa. H-Baba amesema yuko tayari kwa kumpokea mtoto huyo ambaye atakuwa amezaliwa ndani ya ndoa, pichani kama unavyomuona mke wake Flora Mvungi akiwa hoi hiyo ilikuwa jana walivyoenda hosp kucheki hatua za mwisho mwisho.

Ijumaa, 14 Juni 2013

Video ya kwanza iliyomtoa marehemu LANGA ndio hii "MATAWI YA JUU"



(News) Ratiba ya mazishi ya LANGA KILEO




Ratiba ya mazishi ya ndugu yetu Langa Kileo itakuwa kama ifuatavyo, msiba upo nyumbani kwa wazazi wa Langa maeneo ya Mikocheni nyuma ya Hosp ya AAR zamani kulikuwa na ofisi za Benchmark Production. Mwili wa marehemu utaagwa siku ya Jumatatu majira ya saa 7 mchana na baada ya hapo mwili utaelekea makaburi ya Kinondoni kwa mazishi majira ya saa kumi alasiri.

(News) CHAMA CHA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA (TUMA)

                        CHAMA CHA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA TANZANIA (TUMA)
                                  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 14-6-2013

Chama cha muziki wa kizazi kipya Tanzania (TUMA) kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha aliyekuwa msanii mahiri wa Hip Hop nchini marehemu Langa Kileo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye vyombo vya habari,marehemu Langa Kileo alifariki siku ya jana jioni katikia Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipopelekwa kwa ajili ya matibabu.
Tasnia ya muziki nchini imepata pigo lingine tena kwani ni takribani muda wa wiki 2 tokea msanii mwingine mahiri Albert Mangweha afariki Dunia akiwa nchini Afrika Kusini na kuzikwa katika makaburi ya Kihonda yaliyopo Mkoani Morogoro.
Tunapenda kutoa wito kwa wasanii wote nchini kujitokeza kwa wingi na kuonyesha upendo pamoja na kutoa ushirikiano katika kipindi hiki kugumu cha msiba wa msanii mwenzetu Langa Kileo.
Chama kinatoa pole kwa familia ya marehemu,ndugu,jamaa,marafiki na mashabiki wote wa muziki nchini na kuahidi kutoa ushirikiano katika wakati huu mgumu kwetu sote.
Tunaamini tulimpenda lakini Mungu amempenda zaidi,Mungu ampumzishe kwa amani marehemu Langa Kileo.
Amin.
Fredrick Gerson Mariki
Mwenyekiti wa TUMA (TANZANIA URBAN MUSIC ASSOCIATION)

HAPPY BRITHDAY TWALIB KIZIBO