Pages - Menu

Jumatano, 24 Aprili 2013

CPWAA: NGOMA YANGU "REVENGE" NI YA KITAMBO KWENYE ALBUM YA "PWAA THE ALBUM" SIO MPYA IMETOKA BILA RUHUSA YANGU




Inaonekana mtindo wa kutoa ngoma za wasanii bila ruhusa zao umekua kama kawaida siku hizi, wasanii kadhaa wamesikika wakilalamika kazi zao kusikika redioni na kwnye mitandao mbalimbali bila rusa yao, leo hii msanii Ilunga Khalifa aka Cpwaa, ameonekana kushangazwa na ngoma yake "Revenge", kutoka katika album yake "Pwaa The Album" bila ruhusa yake, na kupitia ukurasa wake wa facebook ameomba watu wasichukulie kama ndio ngoma yake mpya, bali ni imetoka bila ruhusa yaken na kuweka sawa kuwa kazi zake mpya zitaanza kusikika kuanzia mwezi wa 7.

CORRECTION: Sijatoa ngoma mpya toka nitoe "Double releases" mwaka jana, najua wengi wameona kwenye blogs mbalimbali kuna ngoma yangu mpya "REVENGE"...well lile pini ni la kitambo na lipo kwenye album yangu ya "Pwaa The Album" iliyotoka mwaka 2011, ngoma ni nyeusi sana sikuiitoa sijui imekuaje imetolewa juzi juzi bila mawasiliano na mimi! Its..ok ila siku ingine tuwasiliane!..Ngoma zangu mpya zitatoka kuanzia mwezi wa 7 mwaka huu..kwa sasa tuko jikoni. Asanteni na tuko pamoja! hakijaharibika kitu ( This is on my behalf of my Management) #Under-Rebranding

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

HAPPY BRITHDAY TWALIB KIZIBO