Pages - Menu

Ijumaa, 14 Juni 2013

Video ya kwanza iliyomtoa marehemu LANGA ndio hii "MATAWI YA JUU"



(News) Ratiba ya mazishi ya LANGA KILEO




Ratiba ya mazishi ya ndugu yetu Langa Kileo itakuwa kama ifuatavyo, msiba upo nyumbani kwa wazazi wa Langa maeneo ya Mikocheni nyuma ya Hosp ya AAR zamani kulikuwa na ofisi za Benchmark Production. Mwili wa marehemu utaagwa siku ya Jumatatu majira ya saa 7 mchana na baada ya hapo mwili utaelekea makaburi ya Kinondoni kwa mazishi majira ya saa kumi alasiri.

(News) CHAMA CHA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA (TUMA)

                        CHAMA CHA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA TANZANIA (TUMA)
                                  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 14-6-2013

Chama cha muziki wa kizazi kipya Tanzania (TUMA) kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha aliyekuwa msanii mahiri wa Hip Hop nchini marehemu Langa Kileo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye vyombo vya habari,marehemu Langa Kileo alifariki siku ya jana jioni katikia Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipopelekwa kwa ajili ya matibabu.
Tasnia ya muziki nchini imepata pigo lingine tena kwani ni takribani muda wa wiki 2 tokea msanii mwingine mahiri Albert Mangweha afariki Dunia akiwa nchini Afrika Kusini na kuzikwa katika makaburi ya Kihonda yaliyopo Mkoani Morogoro.
Tunapenda kutoa wito kwa wasanii wote nchini kujitokeza kwa wingi na kuonyesha upendo pamoja na kutoa ushirikiano katika kipindi hiki kugumu cha msiba wa msanii mwenzetu Langa Kileo.
Chama kinatoa pole kwa familia ya marehemu,ndugu,jamaa,marafiki na mashabiki wote wa muziki nchini na kuahidi kutoa ushirikiano katika wakati huu mgumu kwetu sote.
Tunaamini tulimpenda lakini Mungu amempenda zaidi,Mungu ampumzishe kwa amani marehemu Langa Kileo.
Amin.
Fredrick Gerson Mariki
Mwenyekiti wa TUMA (TANZANIA URBAN MUSIC ASSOCIATION)

Alhamisi, 13 Juni 2013

(News) HABARI ZILIZOTUFIKIA: MSANII WA HIP HOP NCHINI LANGA KILEO AMEFARIKI DUNIA




Habari zilizonifikia sasa hivi punde kutoka kwa ndugu wa karibu wa Langa zinasema ndugu yao Langa amefariki katika hosp kuu ya Muhimbili kwa kuumwa Malaria. Habari kamili zitawajia kwa jinsi nitakavyokuwa napewa updates.
MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI.

Jumamosi, 8 Juni 2013

MR NICE ATEMWA GRANDPA RECORDS AZIKOSA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 141



Baada ya story nyingi kutapakaa, kupitia mitandao mbali mbali hasa ya nchini Kenya, kuwa msanii Mr Nice ametemwa na record iliyokuwa ikimsimamia kazi zake (Grandpa Recods) iliyoko jijini Nairobi kwa kisa cha yeye kupenda pombe, wanawake na kupigana hovyo, kitu kinachopelekea kuchafua picha ya kampuni hiyolakini pia kusahau majukumu yake anayotakiwa kuyakamilisha kama msanii . 255 imeongea na CEO wa Grandpa "Refigah" amethibitisha kuachana na Mr Nice lakini amekanusha sababu zilizotajwa za yeye kuachana na Mr Nice

kuna sababu ndio zilizopelekea kuachana na Mr Nice, la msingi ni msanii hawezi kuwa na management mbili, hawezi kusign contract mbili bila kusema kuhusu contract hiyo nyingine, alikuwa na contract na Sallam pamoja na Lmar na iko active, so sisi kama company tumeamua hapna, tumesitisha kisheria.

kuhusu kusema kuwa wameachana na Mr Nice kwasababu ya ulevi ugomvi na wanawake, amesema kuwa, ni kile midea kinachoripoti lakini yeye kama yeye hajasema kitu kama hicho,na hizo story ni personal na time hii sio time ya kuwa na beef na mtu

ASILIMIA 15 ZA SHOW YA FA "THE FINEST" KUPEWA MAMA WA MAREHEM NGWEA


Baada ya show ya Mwana FA "The Finest" Kuahirishwa wiki iliyopita kutokana na msina wa Rapper Abert Mangwea, aliyefariki jumanne ya tarehe 28 May na kuzikwa siku ya jana Morogoro,
Kama Zamani The Finest,Imetangazwa tena, na safari hii asilimia 15 ya mapato kutoka katika show hiyo, yatapelekwa kwa mama mzazi wa Ngwea.

"nimesema kwamba nitoe hela mfukoni kwangu moja kwa moja, niipeleke huku, kwahiyo chochote nitakacho kipata, nataka kutoa 15 percent nimpelekee bi mkubwa...."amesema Fa

"unajua kitu kama cha kumuita ngwea marehem, bado kilikuwa hakija click kichwani kwangu, hakiji, yaani watu wakimuitwa mangwea marehem naona aaaah, hawa jamaa wanasema vitu gani, bado inanisumbua "

" Nafkiri Pengine sikufanya vyakutosha wakati yuko hai, lakini bado naweza kufanya kitu kama anaona huko aliko naomba awe na moyo mwepesi na mimi, nimeona ntamuandali hiki ambacho nakipata sasa hivi, nimuangalie mama yake, kama ambavyo pengine yeye angefanya kama ingekua album yakwake.amesema mwana FA.

HAPPY BIRTHDAY VANESSA MDEE


jana (tr7) ni siku ya kuzaliwa kwa mwanamuziki na mtangazahi wa Choice Fm, "Vanessa Mdee". Vanessa ndio elifanya collable na Ommy Dimpoz kwenye wimbo uliofanya vizuri sana, mpaka kupelekea kuingia katika tuzo za Killi, zinazotarajiwa kufanyika siku ya leo  Mlimani City. Licha ya collable hiyo, mwenyewe aliachia single yake "Closer" ambayo pia imepata nafasi ya kuingia katika kinyang'anyiro cha tuzo hizo, kupitia category ya msanii anaechipukia. Happy Birthday Vanessa.

ALIETUHUMIWA KUMUUA BABA WA RAP QUEEN KUTOKA KENYA STELA MWANGI AHUKUMIWA



Mwezi wa kwanza mwaka jana, baba mzazi wa Rap Queen kutoka Kenya STL, Mr Jeff Mwangi Kwirikia, aliuwawa baada ya kugongwa na aliemgonga kukimbia katika manispaa ya Ullensaker huko Norway.

Ni zaidi ya mwaka sasa tangu ajali hiyo itokee, na mtuhumiwa huyo kajisalimisha mwenyewe wiki hii kwenye mamlaka husika, hatimae haki kupatikana kwa familia ya STL.

Kutokana na mtandao wa Norway, News In English, dereva huyo amehukumiwa kwa kumgonga kwa bahati mbaya na kumuua Mr. Mwangi katika ajali ya kugonga na kukimbia, na kuhumiwa kifungo cha siku 120 jela siku ya jumanne, lakini pia mahakama hiyo pia imemhukumu mwnaume huyo mwenye miaka 40, kutokuendesha gari tena maishani mwake na zaidi wakamuamuru kuwalipa member wa familia ya mzee Mwangi yenye watu 8 kiasi cha shilingi 35,393,250.00 kwa kila mmoja.

STL, ni mmoja kati ya wale waliofanya show ya uzinduzi wa BBA "The Chase" 2013, wengine ni pamoja nan Wande coal, Don Jazzy pamoja na D’Prince.

CIARA ASHTAKIWA NA BAR YA WATU WENYE KUSHIRIKI MAPENZI YA JINSIA MOJA


Mwanamziki Ciara ameshtakiwa na bar inayohudhuriwa na watu wanyekushiriki mapenzi ya jinsia moja (gay), iliyoko West Hollywood, ambao wanadai kuwa mwanamziki huyo aliwaacha kwenye mataa pale alipojitoa katika moja ya tamasha lao walilotarajia kulifanya leo usiku (7th)

Club hiyo ya usiku inayoitwa "The Factory" inasemekana kuwa inajaza sana wateja wake hao ambao wanajua ku-party

kutokana na mshtaka hayo, Ciara ali-sign dili la dola za kimarekani 10,000 kutokea katika bar hiyo leo usiku, ikiwa ni siku moja kabla ya kufanya show kwenye L.A. Pride parade.

Factory wanasema kuwa Ciara amesema kuwa hataweza ku-perfome kutokana na kizuizi kilichopo kwenye mkataba wake aliosaini na tamasha la Pride na kuendelea kusema kuwa bila kutarajia mwanadada huyo alijitoa siku ya tarehe 3 june, na kuwaacha wakiwa hawana star yoyote kwenye bash hiyo kabla ya pre gay parade bash

Kwasasa bar hiyo inamshtaki Ciara kwa kukatisha mkataba na kumtaka alipe hela zote ilizotumia kutangaza uwepo wake pamoja na pesa ambayo wataikosa kwa kutokuja kwake

HAPPY BRITHDAY TWALIB KIZIBO